#113
Ni Mfalme wa Mapenzi
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ni Mfalme wa mapenzi Ndiye anichungaye, Sipungukiwi, hawezi. Kunipoteza yeye.
Couplet 2
Kando ya mji mazima Yeye huniongoza Katika malisho mema Daima hunilaza.
Couplet 3
Mara nyingi hupotea Kwa ukaidi wangu, Naye huniandamia, Hunirudisha kwangu.
Couplet 4
Uvulini mwa mauti, Siachi hatari kamwe, Wewe Bwana huniachi, Mwokozi wangu wewe.
Couplet 5
Waniandikia meza Neema kwako tele. Kwa wewe, yote naweza. Na Msalaba mbele.
Couplet 6
Kamwe hautapungua Uule wema wako; Mwisho, atanichukua, Juu, niimbe kwako.