#111
Neno lake Bwana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Neno lako, Bwana, Ni imara sana; Lilo latwongoza, Lilo latufunza.
Couplet 2
Adui wabaya Wakikaribia, Neno lake Bwana Ni ulinzi sana.
Couplet 3
Siku za dhoruba Soma ukiomba; Neno lake Bwana Msaada sana.
Couplet 4
Ukiliamini, Hwenda na amani; Una na furaha Neno ni siraha.
Couplet 5
Ni furaha kweli, Na wingi wa mali, Neno lake Bwana Kwa wasiokana
Couplet 6
Neno la rehema, Tukali wazima; Faraja I papo, Tufarikanapo.
Couplet 7
Tulijue sana Neno lako, Bwana, Hapa tupende, Kisha kwako twende.