Indirimbo Zikundwa Open in the app

#110

Mapya ni mapenzi hayo

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Mapya ni mapenzi hayo, Asubuhi tunayo, Saa za giza hulindwa Kwa uzima kuamshwa.

Couplet 2

Kila siku, Mapya pia Rehema, wema, na afya, Wokofu, na msamaha, Mawazo mema, furaha.

Couplet 3

Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao, Mungu atatueleza Yatakayompendeza.

Couplet 4

Mambo yetu ya dunia Mungu atayang’aria, Matata atageuza Yawe kwetu ya Baraka.

Couplet 5

Yaliyo madogo, haya Mungu tukimfanyia, Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.

Couplet 6

Ewe Bwana, siku zote, Tusaidie kwa yote: Mwendo wetu wote vivyo, Uwe kama tuombavyo.