Indirimbo Zikundwa Open in the app

#109

Nitaimba ya Yesu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nitaimba ya Yesu, Kwa rehema zake, Baraka nyingi sana Nimepata kwake; Nitaimba ya Yesu, Sadaka ya Mungu, Alimwaga damu Ukombozi wangu.

Couplet 2

Nitaimba ya Yesu Hapa siku zote, Nitakapokumbuka Vyema vyake vyote; Nitaimba ya Yesu Hata mashakani, Yeye atanilinda Mwake ubavuni.

Couplet 3

Nitaimba ya Yesu Niwapo Njiani; Takaza Mwendo, hata Nifike Mbinguni; Nikiisha ingia Mlangoni mle, Yesu nitamwimbia Mbinguni milele.