#104
Twasoma ni njema sana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Twasoma, ni njema sana Mbinguni, kwa Bwana; Twasoma, dhambi hapana, Mbinguni kwa Bwana; Malaika wema wako, Vinanda vizuri viko, Na majumba tele yako, Mbinguni kwa Bwana.
Couplet 2
Siku zote ni mchana, Ni nchi ya raha; Wala machozi hapana, Ni nchi ya raha; Walioko wanuona Uso wa Mwokozi, tena Jua jingine hapana, Ni nchi ya raha.
Couplet 3
Nyama na vitu viovu Havimo kabisa; Kifo nacho, na ubovu, Havimo kabisa. Ni watakatifu wote, Wameoshwa dhambi zote; Wasiosafiwa wote Hawamo kabisa.
Couplet 4
Tuna dhambi, pia sote, Mwokozi akafa; Kwake tutaoshwa zote, Mwokozi akafa; Kwake twapata Wokovu, Tutawona utukufu; Mbinguni tutamsifu; Mwokozi akafa.
Couplet 5
Baba, mama, ndugu zetu, Twendeni kwa Bwana; Huku chini sio kwetu, Twendeni kwa Bwana; Tusishikwe na dunia, Na dhambi kutulemea; Tutupe vya chini pia, Twendeni kwa Bwana.