#105
Kuwatafuta
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Kuwatafuta wasioweza, Kuomba wamrejee Yesu, Kuwaambia maneno yake, “Njooni kwangu, nawapenda”.
Refrain
Nitakwenda, (kwenda), niwatafute Waongofu (wa Bwana) wageuke, Waingie (wote) katika zizi La Mkombozi (wetu) Yesu Kristo.
Couplet 2
Kuwatafuta wasioweza, Waonyeshwe Mwokozi wetu, Kuwaongoza, wapate wote Uzima wa milele.
Refrain
Nitakwenda, (kwenda), niwatafute Waongofu (wa Bwana) wageuke, Waingie (wote) katika zizi La Mkombozi (wetu) Yesu Kristo.
Couplet 3
Kazi hiyo nataka kufanya, Leo nimesikia mwito Kuwainua waangukao, Waletwe kwake Yesu njia.