#103
Kaa nami
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Kaa nami, ni usiku tena; Usiniache gizani, Bwana; Msaada wako haukomi; Nili peke yangu, kaa nami.
Couplet 2
Siku zetu hazikawi kwisha, Sioni la kunifurahisha; Hakuna ambacho hakikomi, Usiye na mwisho kaa nami.
Couplet 3
Nina haja nawe kila saa; Sina mwingine wa kunifaa; Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe? Bwana, kaa name.
Couplet 4
Sichi neno uwapo karibu; Nipatalo lote, si taabu; Kifo na kaburi haviumi; Nitashinda kwako, kaa nami.
Couplet 5
Nilalapo nikuone wewe, Gizani mote nimulikiwe; Nuru za Mbinguni hazikomi, Siku zangu zote kaa nami.