#102
Kazi yangu ikiisha
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; Na kuvaa kutokuharibika, Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni; Atakuwa wa kwanza kunilaki.
Refrain
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Couplet 2
Furaha nitapata nikiona makao Bwana aliyotuandalia; Nitamsifu Mwokozi kwa rehema na pendo Vilivyonipa pahali Mbinguni.
Refrain
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Couplet 3
Nao waliokufa katika Bwana Yesu, Nitawaona tena huko juu; Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Refrain
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Couplet 4
Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha, Pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Refrain
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.