#99
Maelfu na maelfu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Maelfu na maelfu Wenye nguo bora! Masafu ya waongofu Wenye na bendera! Amekwisha kamili Vita vya Shetani Fungueni lango hili; Njoni, ingieni!
Couplet 2
Imbeni aleluya, Zipae Mbinguni! Pigeni sana sauti Kwa kutumaini! Kwa hiyo viliumbwa Nchi hata Mbingu Dhiki za muda zikisha, Asifiwe Yesu.
Couplet 3
Loo! Tukionana Pwani ya ng’amboni! Loo! Tukishirikiana Milele Mbinguni! Midomo yote pia, Huko itaimba Wajane kufufukiwa Na kila yatima!
Couplet 4
Himiza enzi yako, Uliyetufia Utimize watu wako, Wakosaji pia, Mpendwa wa taifa twakutumaini! Uzifunue ishara Urudi enzini!