#100
Safari Tumrudie Bwana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mbona washangaa njiani? Mbona warejea nyuma? Warudi tena gizani Alimokutoa Bwana?
Couplet 2
Ni ya bure yote haya, Uliyofunzwa ya Mungu? Ni bure amekufia Bwana Yesu kwa uchungu?
Couplet 3
Wamtia Kristo aibu Na maneno yake pia? Siku yaja ya hesabu, Utamjibuje Bwana?
Couplet 4
Upandapo tena hayo, Halafu utayavuna. Rudi kwa Bwana upesi, Mwombe akupokee tena.