Indirimbo Zikundwa Open in the app

#98

Huyo ndiye anashuka

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Huyo ndiye! anaskuka, Aliyetufilia, Wengi waliookoka, Wakimfurahia, Aleluya! Yesu aturudia.

Couplet 2

Sote tutamtazama, Amekaa kitini, Nao waliomcoma, Kumkaza mtini, Na kilio, wamuone enzini.

Couplet 3

Alama za kifo chake Hata sasa anazo Na waaminifu wake Wapendezewa nazo. Alipata, Kwetu alama hizo.

Couplet 4

Wokovu utakiwao Sasa wapatikana, Na watakatifu hao Mbinguni wakutana Kumlaki, Ndiyo siku ya Bwana

Couplet 5

Wakusujudie wote Mbele ya kiti chako. Zako, Bwana, nguvu zote Itwae milki yako Njoo Bwana, Sisi tu watu wako.