Indirimbo Zikundwa Open in the app

#97

Tazameni huyo ndiye

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Tazameni huyo ndiye, Mwenye kushinda vita; Haya, tumsujudie; Nyara anazileta; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini.

Couplet 2

Msifuni malaika, Mtukuzeni sana, Wote waliookoka Watamsifu Bwana; Watu wote msifuni, Sasa yumo kitini.

Couplet 3

Walimfanya dhihaka Zamani wenye shari, Kwao waliookoka Ni Bwana wa fahari; Watu wote msifuni. Sasa yumo Kitini.

Couplet 4

Nyimbo nzuri, sikizeni, Ni nyimbo za sifa kuu, Za Bwana Yesu kitini, Kutawazwa, yeye tu; Watu wote msifuni Sasa yumo Kitini.