Indirimbo Zikundwa Open in the app

#96

Mle kaburini, Yesu Mwokozi

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Mle kaburini, Yesu Mwokozi! Alilazwa chini, Bwana wangu!

Refrain

Bwana! Amefufuka, Kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, Sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai!

Couplet 2

Aungoja huo, Yesu Mwokozi! Mchana ujao, Bwana wangu!

Refrain

Bwana! Amefufuka, Kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, Sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai!

Couplet 3

Walinda kaburi, Yesu Mwokozi! Bure ni muhuri, Bwana wangu!

Refrain

Bwana! Amefufuka, Kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, Sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai!

Couplet 4

Kifo kimeshindwa, Yesu Mwokozi! Pingu zimevunjwa, Bwana wangu!