#91
Mapenzi yako yafanyike, Bwana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mapenzi yako yafanyike, Wewe mfinyanzi, nami towe, Unifinyange upendavyo, Mimi tayari, naja kwako.
Couplet 2
Mapenzi yako yafanyike, Unihoji dhambi zote, Unisafishe vya kimwili, Niinamapo Msalabani.
Couplet 3
Mapenzi yako yafanyike, Mimi dhaifu, mimi mnyonge. Uwezo wote, kwako kweli, Sasa niponye, Ee, Mwokozi.
Couplet 4
Mapenzi yako yafanyike, Natoa kwako vitu vyote, Maisha, mali, moyo, mwili, Vyote ni vyako, kweli, kweli.
Couplet 5
Mapenzi yako yafanyike, Mapenzi yangu yavunjike, Ninakubali uwe Bwana, Ni mali yako, twaa kabisa.
Couplet 6
Mapenzi yako yafanyike, Unitawale siku zote, Sura ya Yesu umba kwangu, Nijaze Roho nayo nguvu.