Indirimbo Zikundwa Open in the app

#92

Nataka nimjue Yesu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Nataka nimjue Yesu, Na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.

Refrain

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.

Couplet 2

Nataka nione Yesu, Na nizidi kusikia, Anenapo kitabuni, Kujidhihirisha kwangu.

Refrain

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.

Couplet 3

Nataka nifahamu, na Nizidi kupambanua Mapenzi yake, nifanye Yale yanayompendeza.

Refrain

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.

Couplet 4

Nataka nikae naye, Kwa mazungumzo zaidi, Nizidi kuwaonyesha Wengine Wokovu wake.

Refrain

Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.