#90
Aliteswa, aliteswa
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Aliteswa, aliteswa, Msalabani Yesu aliteswa, Dhambi zangu ameziondoa, Mahali pangu aliumizwa.
Couplet 2
Alikufa, alikufa, Msalabani Yesu alikufa, Kwa kifo chake nakombolewa, Kwa kuwa Yesu alinifia.
Couplet 3
’Kafufuka, ‘kafufuka, Kaburini Yesu alitoka, Nami nimewekwa huru pia, kwa kuwa Yesu alifufuka.
Couplet 4
Yuko hai, yuko hai, Mbinguni anaishi Mwombezi, Daima huniombea mimi, Kwa kuwa Yesu adumu hai.
Couplet 5
Atarudi, atarudi, Siku moja Yesu atarudi, Na tutamwonapo tutafurahi, Kwa kupelekwa kwake Mbinguni.
Couplet 6
Sifa kwake, sifa kwake, Mbinguni na huimbwa milele, Kwa furaha, masifu, na shangwe, Tutamwimbia Yesu milele.