#89
Kwa Kalvari
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Muda mwingi nilipotea, Sikufahamu Msalaba, Wala aliyenifilia, Kwa Kalvari.
Refrain
Rehema bure na neema, Samaha nalo nilipewa, Ndipo aliponifungua Kwa Kalvari.
Couplet 2
Kwa neno lake Bwana Mungu, Nilijiona mimi mwovu, Nikageuka na kutubu, Kwa Kalvari.
Refrain
Rehema bure na neema, Samaha nalo nilipewa, Ndipo aliponifungua Kwa Kalvari.
Couplet 3
Yote kwa Yesu namtolea, Ndiye mfalme wa pekee sasa, Kwa furaha nitamwimbia, Wa Kalvari.
Refrain
Rehema bure na neema, Samaha nalo nilipewa, Ndipo aliponifungua Kwa Kalvari.
Couplet 4
Jinsi Pendo lilivyo kuu, Neema ilishuswa toka juu, Alitufanyia Wokovu Kwa Kalvari.