#88
Ndiyo damu ya Baraka
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa, Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa; Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa; Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa.
Refrain
Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe katika damu; Takuwa safi kabisa.
Couplet 2
Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini, Na maumivu si haba yaliyompata chini. Nataka kijito hicho niende kuoga sasa; Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.
Refrain
Safi kabisa; safi kabisa! Ndicho kinitakasacho, Nami ni safi kabisa.
Couplet 3
Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu; Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi Wokovu? Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa; Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa.
Refrain
Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe kwa damu yako, Nami ni safi kabisa.