#87
Deni ya dhambi ilimalizika
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa. Kwake Msalabani Nilipewa uzima.
Refrain
Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.
Couplet 2
Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu, Uwezo wa ushindi Hupatikana kwangu.”
Refrain
Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.
Couplet 3
Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe.
Refrain
Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.
Couplet 4
Sina wema moyoni, Nidai neema, Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa.
Refrain
Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.
Couplet 5
Hata huko Mbinguni Miguuni pake, “Yesu alinifia,” Nitaimba milele.
Refrain
Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.