Indirimbo Zikundwa Open in the app

#86

Damu imebubujika

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Damu imebubujika, Ni ya Imanweli, Wakioga wenye taka, Husafiwa kweli.

Couplet 2

Ilimpa kushukuru Mwivi mautini; Nami nisiye udhuru, Yanisafi ndani.

Couplet 3

Kondoo wa kuuawa, Damu ina nguvu, Wako wote kuokoa, Kwa utimilivu.

Couplet 4

Bwana tangu damu yako Kunisafi kale, Nimeimba sifa zako; Taimba milele.

Couplet 5

Nikifa tazidi kwimba Sifa za Wokovu Ulimi ujaponyamaa Vumbini mwa ufu.

Couplet 6

Bwana, umenikirimu Nisiyestahili Kwa damu yako, sehemu Ya mali ya kweli.

Couplet 7

Nikubali kukwimbia, Mbinguni milele, Mungu nitakusifia Jina lako pweke.