Indirimbo Zikundwa Open in the app

#85

Ni mtu wa simanzi

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ni “Mtu wa Simanzi”, Mwana wa mwenye enzi Mwenye mengi mapenzi! Asifiwe Bwana Yesu!

Couplet 2

Akawa matesoni, “Mungu mwana yakini Akatoka Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!

Couplet 3

Akapata dhihaka, Mzoea – mashaka Ndiye yetu sadaka: Asifiwe Bwana Yesu!

Couplet 4

Tu wenye dhambi sana; Kwake dhambi hamna, Na Mungu twapatana: Asifiwe Bwana Yesu!

Couplet 5

Alikufa mtini, Akalia dhikini, Sasa yuko Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!

Couplet 6

Punde atarejea, Yesu kutunyakua, Ndipo tutamwimbia: Asifiwe Bwana Yesu!