Indirimbo Zikundwa Open in the app

#84

Niwonapo mti bora

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Niwonapo mti bora Kristo aliponifia Kwangu pato ni hasara Kiburi nakichukia.

Couplet 2

Na nisijivune, Bwana Ila kwa mauti yako; Upuzi sitaki tena, Ni chini ya damu yako.

Couplet 3

Tangu kichwa hata nyayo, Zamwagwa pendo na hamu, Ndako pweke hamu hiyo, Pendo zako zimetimia.

Couplet 4

Vitu vyote vya dunia, Si sadaka ya kutosha; Pendo zako zinawia Nafsi, mali, na maisha.