Indirimbo Zikundwa Open in the app

#83

Kwa wingi wa nyama

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Kwa wingi wa nyama, Na sadaka pia, Hupata wapi salama, Kwondoa hatia?

Couplet 2

Sadaka ni Yesu, Hwondoa makosa; Dhabihu mwenye jina kuu, Atanitakasa.

Couplet 3

Kwa yangu imani, Nikuweke sasa Mkono mwako kichwani Kukiri makosa.

Couplet 4

Roho yakumbuka Mambo ya mtini, Mzigo ulijitweka, Ndiyo yangu deni.

Couplet 5

Deni hutanguka, Tukimuamini; Kwa damu tumeokoka, Twimbe furahani.