#82
Sioni haya kwa Bwana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Sioni haya kwa Bwana Kwake nitang’ara! Mti wake sitakana, Ni neno imara!
Refrain
Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo; Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo.
Couplet 2
Kama kiti chake vivyo Ni yake ahadi, Alivyowekewa navyo Kamwe havirudi.
Refrain
Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo; Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo.
Couplet 3
Bwana wangu, tena Mungu Ndilo lake jina! Hataacha roho yangu Wala kunikana.
Refrain
Msalaba ndio asili ya mema, Nikatua mzigo hapo; Nina uzima, furaha daima, Njoni kafurahini papo.
Couplet 4
Atakiri langu jina, Mbele za Babaye, Anipe pahali tena Mbinguni nikae.