Indirimbo Zikundwa Open in the app

#81

Chini ya Msalaba

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Chini ya Msalaba Nataka simama; Ndio mwamba safarini, Wa kivuli chema; Ni kweli kwa roho yangu Ni tuo kamili, Tatua mzigo wangu Wakati wa hari.

Couplet 2

Hapa ni pema sana, Ni ngome kamili; Hapa yameonekana, Mapenzi ya kweli; Kama alivyoonyeshwa Yakobo zamani, Msalaba umekuwa Ngazi ya Mbinguni.

Couplet 3

Na Yesu Msalabani Walimkemea, Alikufa niokoke Niliyepotea; Naona ajabu sana Ya mambo mawili Jinsi alivyonipenda, Nisiyestahili.

Couplet 4

Atakayeonana, Na Yesu Mbinguni, Njia yake aanzapo Ni Msalabani; Wokovu upo hapa tu, Mwingine hapana, Kisha kuna furaha kuu Pamoja na Bwana.