Indirimbo Zikundwa Open in the app

#80

Wamwendea Yesu kwa kusafiwa

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Wamwendea Yesu kwa kusafiwa, Na kuoshwa kwa damu ya kondoo? Je neema yake umemwagiwa, Tumeoshwa kwa damu ya kondoo?

Refrain

Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

Couplet 2

Wamwandama daima mkombozi Na kuoshwa na damu ya kondoo? Yako kwa msulubiwa makazi, Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

Refrain

Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

Couplet 3

Atakapokuja Bwana –arusi Uwe safi kwa damu ya kondoo! Yafae kwenda Mbinguni mavazi Yafuliwe kwa damu ya kondoo.

Refrain

Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo?

Couplet 4

Yatupwe yaliyo na takataka, Na uoshwe kwa damu ya kondoo. Huoni kijito chatiririka Na uoshwe kwa damu ya kondoo?

Refrain

Kuoshwa, kwa damu, Itutakasayo ya kondoo; Ziwe safi nguo nyeupe mno; Umeoshwa kwa damu ya kondoo?