Indirimbo Zikundwa Open in the app

#79

Msalaba wa aibu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Msalaba wa aibu, Ulinipa amani; Uliniondoa kifungoni, Nilimotesekea.

Couplet 2

Ee, Mwokozi wangu, Yesu Nitamwendea nani? Najiweka Msalabani, Nikaoshwe damuni.

Couplet 3

Nakupenda Bwana Yesu, Kwa kunipenda kwako, Napendezwa nikutumikie Maisha yangu yote.

Couplet 4

Usifiwe Bwana Yesu, Kwa ulivyonifia, Aleluya, nakushukuru, Uliyenikomboa.

Couplet 5

Msalaba ulishinda Nguvu zake adui, Ili mimi nikombolewe, Niwe mwana wa Mungu.