#78
Sioshwi dhambi zangu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Sioshwi dhambi zangu, Bila damu yake Yesu. Hapendezewi Mungu, Bila damu yake Yesu.
Refrain
Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.
Couplet 2
La kunisafi sina Ila damu yake Yesu. Wala udhuru tena, Ila damu yake Yesu.
Refrain
Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.
Couplet 3
Sipati pataniswa, Bila damu yake Yesu. Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu.
Refrain
Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.
Couplet 4
Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu. Wema wala amani, Bila damu yake Yesu.
Refrain
Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.
Couplet 5
Yashinda ulimwengu, Hiyo damu yake Yesu. Na kutufikisha juu, Hiyo damu yake Yesu.
Refrain
Hakuna kabisa Dawa ya makosa Ya kututakasa, Ila damu yake Yesu.
Couplet 6
Twaimba: Utukufu Una damu yake Yesu. Milele twaisifu, Hiyo damu yake Yesu.