#77
Msalabani pa Mwokozi
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Msalabani pa Mwokozi, Hapo niliomba upozi, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Refrain
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Couplet 2
Chini ya mti msumbufu, Niliomba utakatifu, Alinikomboa kwa damu, Mwana wa Mungu.
Refrain
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Couplet 3
Aliniokoa dhambini, Ikawa kunikaa ndani, Aliponifia mtini, Mwana wa Mungu.
Refrain
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Couplet 4
Damu ya Yesu ya thamani, Huniokoa makosani, Huniendesha Wokovuni, Mwana wa Mungu.
Refrain
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.
Couplet 5
Hicho kijito cha gharama, Leo jivike kwa kuzama, Kwake uuone uzima, Mwana wa Mungu.
Refrain
Mwana wa Mungu, Mwokozi wangu, Akaniokoa mpenzi, Mwana wa Mungu.