Indirimbo Zikundwa Open in the app

#76

Njoni, enyi wa imani

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Njoni na furaha, enyi wa imani, Njoni Bethilehemu upesi ! Amezaliwa jumbe wa Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.

Couplet 2

Mungu wa waungu, Mwanga wa mianga, Amekuwa radhi kuzaliwa; Mungu wa kweli, wala si kiumbe; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.

Couplet 3

Jeshi la Mbinguni, Imbeni kwa nguvu, Mbingu zote na zijae sifa; Sifuni Mungu aliye Mbinguni; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.

Couplet 4

Ewe Bwana mwema, twakubarikia, Yesu, utukufu uwe wako; Neno la Baba limekuwa mwili; Njoni tumuabudu, njonu tumuabudu, Njoni tumuabudu Mwokozi.