Indirimbo Zikundwa Open in the app

#75

Waimba, sikizeni

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni; Wimbo wa tamu sana Wa pendo zake Bwana, “Duniani salama, Kwa wakosa rehema.” Sisi sote na twimbe Nao wale wajumbe; Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.

Couplet 2

Ndiye Bwana wa Mbingu, Tangu milele Mungu, Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali; Ametoka enzini Kuja ulimwenguni Mwokozi atufie, Ili tusipotee. Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.

Couplet 3

Mtukufu wa amani Ametoka Mbinguni, Jua la haki, ndiye Atumulikiaye; Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi, Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya, Waimba sikizeni, Malaika Mbinguni.

Couplet 4

Njoo upesi, Bwana, Twakutamani sana; Kaa nasi, Mwokozi Vita hatuviwezi; Vunja kichwa cha nyoka, Sura zako andika, Tufanane na wewe, Kwetu sifa upewe, Waimba, sikizeni, Malaika Mbinguni.