#74
Wachunga walipolinda
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Wachunga walipolinda Kucha nyama zao, Malaika mtukufu Alishuka kwao.
Couplet 2
Wakacha sana wachunga, Akawatuliza, “Nawaletea habari Ya kuwapendeza.”
Couplet 3
”Mji ule wa Daudi Leo amezawa Mwokozi ni Kristo Bwana, Ilivyoandikwa”.
Couplet 4
”Huyo mwana wa Mbinguni Ataonekana, Amelazwa kihorini Malazi hapana.”
Couplet 5
Alipokwisha yanena Malaika hao Waliimba wimbo huu Usio na mwisho:
Couplet 6
”Enzi ni yake Munju juu, Na nchi salama, Kwa watu nao radhi kuu, Sasa na daima.”