Indirimbo Zikundwa Open in the app

#73

Yesu zamani Bethilehemu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu zama Bethilehemu, Aliyezaliwa kwa aibu, Ndiye mwakozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi.

Refrain

Akaja kwa mimi; akaja kwa mimi; Ndiye mwaokozi wa ulimwengu, Akaja kwa mimi.

Couplet 2

Yesu akafa Msalabani, Kuniponya akalipa deni, Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi!

Refrain

Kunifia mimi! Kunifia mimi! Ni la ajabu ya jinsi gani Kunifia mimi.

Couplet 3

Ni yeye huyo tangu asili; Na nilipotanga-tanga mbali Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi.

Refrain

Kuniita mimi; Kuniita mimi; Alikuja kwa upole, kweli Kuniita mimi.

Couplet 4

Yesu Kristo Atarudi tena, Hilo lanifurahisha sana. Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi.

Refrain

Kunijia mimi, kunijia mimi, Yeye Bwana akionekana Kunijia mimi.