#72
Twendeni! Haraka!
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno Liwe mwanga kwa nchi zilizo giza. Bwana alisema nendeni po pote Kawafundisheni mataifa yote. Pelekeni Injili kwa jina la Yesu. Upesi! Twendeni haraka!
Couplet 2
Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La upendo wa Mungu kwa watu wote; Aliyeupenda sana ulimwengu Akamtoa Yesu Mwana wake pekee Kaleta Wokovu, tumtangazeni. Upesi! Twendeni haraka!
Couplet 3
Twendeni! Haraka! Tupeleke Neno La uzima kwa watu waliokufa. Mateka ya Shetani litafungua Litaponyesha na kuwapa amani. Twendeni upesi, tukawaokoe. Upesi! Twendeni haraka!