Indirimbo Zikundwa Open in the app

#69

Twendeni Askari

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Twendeni Askari, watu wa Mungu; Yesu yuko mbele, tumwandame juu. Ametangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini.

Refrain

Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Couplet 2

Jeshi la Shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia, Kelele za shangwe zivume nchi; Ndugu inueni zenu sauti.

Refrain

Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Couplet 3

Kweli kundi dogo, watu wa Mungu Sisi na mababa tu moja fungu. Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini moja, na moja dini.

Refrain

Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

Couplet 4

Haya mbele watu nasi njiani, Inueni myoyo, nanyi sifuni; Heshima na sifa ni ya Mfalme, Juu hata chini, sana zivume.

Refrain

Twende askari watu wa Mungu; Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.