Indirimbo Zikundwa Open in the app

#70

Yesu Atuchunga

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu Atuchunga, Mchunga wetu, Naye atufuta Machozi yetu; Mkononi mwake Hatuna hofu, Daima twapata Kwake Wokovu.

Couplet 2

Yesu atuchunga Tumemjua, Na sauti yake Twaitambua; Naye akituonya Ni kwa upole, Tu kondoo zake Hata milele.

Couplet 3

Yesu atuchunga; Aliwafia Kondoo wakubwa Na wana pia; Kwamba awajua, Kondoo zake, Hutiwa alama Ya damu yake.

Couplet 4

Yesu atuchunga; Mikono yake Imewaambata Kondoo zake; Hapati wadhuru Adui yule, Yesu Awalinda.