#68
Mungu Msaada wetu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mungu Msaada wetu Tangu myaka yote, Ndiwe tumaini letu La zamani zote.
Couplet 2
Kivuli cha kiti chako Ndiyo ngome yetu. Watosha mkono wako Ni ulinzi wetu.
Couplet 3
Kwanza havijakuwako Nchi na milima, Ndiwe Mungu; chini yako Twakaa salama.
Couplet 4
Na myaka elfu ni kama Siku moja kwako; Utanilinda daima Tu wenyeji wako.
Couplet 5
Binadamu huondoka, Mwisho hana kitu; Kama ndoto hutoweka Ndivyo hali yetu.
Couplet 6
Ila wewe Mungu wetu Ndiwe wa kudumu; Ndiwe bora, ngome yetu Twakaa dawamu.