Indirimbo Zikundwa Open in the app

#67

Bwana uliyewaita

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Bwana uliyewaita Watakatifu wako, Wawe mitume, wachunga, Walishe kundi lako; wanyonge na wenye hofu Wakawa mashujaa, Na wapole wa kunena Wasiwe kunyamaa.

Couplet 2

Hata leo wawataka Watakatifu wako, Nawe wauliza tena Ni nani aliyeko Atakaye nimtume Afundishe vijana? “Ni tayari, Bwana wangu, Nitume mimi Bwana.”

Couplet 3

Nitume na mimi, Bwana Kama ulivyotumwa, Habari ya msamaha Na dhambi kutubiwa, Niwahubiri wakosa, Na waliopotea, Wokovu u wake Bwana, Aliyewafilia.

Couplet 4

Astahiliye hapana Kutamka habari, Lakini wewe waweza Kutufanya tayari. Neno lako tulijue, Tupe na roho yako, Hayatakuwa ya bure, Haya maneno yako.