#66
Po pote mashamba yajaa
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Po pote mashamba yajaa, Tele nafaka pevu, Po pote yang’aa meupe Bondeni na nyandani.
Refrain
Mwenye mavuno, wasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe.
Couplet 2
Wapeleke uchaoni, Waende na jotoni, Mpaka jua lishukapo Wakusanye ko kote.
Refrain
Mwenye mavuno, wasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe.
Couplet 3
Watenda kazi wa Bwana, Mlete sasa mazao, Na jioni ingieni Kwake na furaha kuu.
Refrain
Mwenye mavuno, wasihi Upeleke wavuni, Wakusanye mazao, Hata kazi iishe.