#59
Peleleza ndani yangu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Peleleza ndani yangu, Iwe safi nia, Kwangu kama kwako Mungu, Idhihiri pia.
Couplet 2
Peleleza moyo wangu Uunifunulie, Yaliyomo ndani yangu Nami niyajue.
Couplet 3
Kwanza washe zako tambi, Kumefunga giza; Nijue ambavyo dhambi Ni la kuchukiza.
Couplet 4
Peleleza na mawazo Ni mbegu za mambo, Asili ya machukizo, Maumbuo – umbo.
Couplet 5
Zidi kuyapeleleza Katikati yangu Hata wishe nifundisha Udhaifu wangu.
Couplet 6
Hapo nikikwinamia Mbele zako, Mungu, Hakika nitakujua U mpenzi wangu.