Indirimbo Zikundwa Open in the app

#60

Waponyeni watu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Waponyeni watu wamo kifoni, Watoeni walio shimoni; Na aangukaye mumzuie; Ya Bwana Yesu wahubirini.

Refrain

Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini.

Couplet 2

Wajapokawia anangojea, Awasubiri waje tobani; Msiwadharau, muwaonyeni; Huwasamehe; wakiamini.

Refrain

Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini.

Couplet 3

Myoyoni mwa ndani, yule Shetani Ameyaseta mawazo yao; Lakini kwa Bwana huwa mazima, Tukiwavuta kwa pole hao.

Refrain

Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini.

Couplet 4

Kawaokoeni, wale njiani, Mutimize mapenzi ya Bwana; Na kwa nguvu zake warudi kwake, Kwa subira waonyeni sana.

Refrain

Walio kifoni waokoeni, Mwokozi yuko, wahubirini.