#58
Mwamba wenye imara
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mwamba wenye imara Kwako nitajificha! Maji hayo na damu Yaliyotoka humu, Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi.
Couplet 2
Kwa kazi zote pia, Sitimizi sharia. Nijapofanya bidii, Nikilia nakudhii, Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa.
Couplet 3
Sina cha mkononi, Naja Msalabani; Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike; Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.
Couplet 4
Nikungojapo chini, Nakwenda kaburini; Nipaapo Mbinguni, Na kukwona enzini: Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe.