#57
Naendea Msalaba
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Naendea Msalaba, Ni mnyonge na mpofu, Yapitayo naacha, Nipone Msalabani.
Refrain
Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, mponya wangu.
Couplet 2
Nakulilia sana: Nalemewa na dhambi; Pole Yesu asema; “Nitazifuta zote”.
Refrain
Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, mponya wangu.
Couplet 3
Natoa vyote kwako, Nafasi nazo nguvu, Roho yangu na mwili, Viwe vyako milele.
Refrain
Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, mponya wangu.
Couplet 4
Kwa damu yake sasa, Nimegeuka roho, Nikaziacha tama Nimfuate Yesu tu.
Refrain
Nakutumaini tu, Ewe Mwana wa Mungu; Nainamia kwako; Niponye, mponya wangu.
Couplet 5
Yesu yuaja tena! Nimepevuka kwake, Kila chembe kamili; Msifuni yeye mponya!