Indirimbo Zikundwa Open in the app

#56

Ni sikukuu siku ile

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ni siku kuu siku ile Ya kumkiri Mwokozi! Moyo umejaa tele, Kunyamaza hauwezi.

Refrain

Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.

Couplet 2

Tumekwisha kupatana Mimi wake, yeye wangu, Na sasa nitamwandama, Nikiri neno la Mungu.

Refrain

Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.

Couplet 3

Moyo tulia kwa Bwana Kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena; Yesu ndiye njia yako.

Refrain

Siku kuu! Siku kuu! Ya kuoshwa dambi zangu kuu! Hukesha na kuomba tu, Ananiongoza miguu. Siku kuu! siku kuu! Ya kuoshwa dhambi zangu kuu.

Couplet 4

Nadhiri yangu ya mbele Nitaiweka daima, Hata ije siku ile, Ya kwonana kwa Salama.