#55
Nipe moyo wenye sifa
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Nipe moyo wenye sifa Sio wa utumwa; Moyo ulionyunyizwa Damu ya thamani.
Couplet 2
Moyo msikizi, moyo Wa kunyenyekea, Moyo utawaliwao Na Mwokozi pia.
Couplet 3
Mwenye kutubu, mnyonge, Sadiki, amini; Kamwe, kamwe asitengwe Akaaye ndani.
Couplet 4
Mpya, mwema na mawazo Mwingi wa mapenzi Nawe uwe kielelezo Moyo wa Mwokozi.
Couplet 5
Ni uule moyo wako; Moyo wa huruma Yesu, natamani kwako Kukujua vyema.
Couplet 6
Na ya midomo matunda Yako, nipe nami; Amani isiyokoma Iwe yangu mimi.
Couplet 7
Nitie yako tabia, Inishukie juu; Jina lako nipe pia, Ndilo la upendo.
Couplet 8
Ni wa baba utukufu; Mwana atukuke; Na roho Mtakatifu U utatu pweke.