#54
Yesu nataka kutakaswa sana
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Yesu nataka kutakaswa sana, Nataka moyo uwe enzi yako. Ukiangushe kilichoinuka Unioshe sasa niwe mweupe.
Refrain
Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.
Couplet 2
Bwaba Yesu, unitazame sasa, Unifanye niwe dhabihu hai; Najitoa kwako, na moyo wote; Unioshe sasa niwe mweupe.
Refrain
Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.
Couplet 3
Bwana kwa hiyo nakuomba sana, Nakungojea miguuni pako, Naomba unioshe damuni tu, Unioshe sasa niwe mweupe.
Refrain
Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.
Couplet 4
Bwana nidumu kukungojea, Niumbie moyo safi, Ee Mungu, Wanaokujia hutupi kamwe, Unioshe sasa niwe mweupe.
Refrain
Mweupe tu, ndiyo mweupe, Ukiniosha nitakuwa safi.