#49
Nitwae hivi nilivyo
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Nitwae hivi nilivyo, Umemwaga damu yako, Nawe ulivyoniita, Bwana Yesu, naja, naja.
Couplet 2
Hivi nilivyo; si langu Kujiosha roho yangu; Nisamehe dhambi zangu, Bwana Yesu, naja, naja.
Couplet 3
Hivi nilivyo; sioni Kamwe furaha moyoni; Daima ni mashakani, Bwana Yesu, naja, naja.
Couplet 4
Hivi nilivyo kipofu, maskini na mpungufu; Wewe u mtimilifu; Bwana Yesu, naja, naja.
Couplet 5
Nawe hivi utanitwaa; Nisithubutu kukawa, Na wewe hutanikataa, Bwana Yesu, naja, naja.
Couplet 6
Hivi nilivyo; mapenzi Yamenipa njia wazi; Hali na mali sisazi, Bwana Yesu, naja, naja.