Indirimbo Zikundwa Open in the app

#50

Yesu nakupenda, U mali yangu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Yesu nakupenda, U mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu; Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Couplet 2

Moyo umejaa mapenzi tele Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Couplet 3

Ulipoangikwa Msalabani Tusamehewe tulio dhambini; Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Couplet 4

Niwapo hai, niwapo maiti, Kupendana nawe kamwe siachi; Hari za kifo zikinienea, Sasa nakupenda, kuzidi pia.

Couplet 5

Mawanda mazuri, na masikani Niyatazamapo huko Mbinguni, Tasema na taji nitakayovaa Sasa nakupenda, kuzidi pia.