#48
Naweka dhambi zangu
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Naweka dhambi zangu Juu yake Bwana Kuziondoa, kwangu Hulemea sana; Na uaili wangu Ameuondoa; Dawa yangu ni damu, Kwa hiyo napoa.
Couplet 2
Na uhitaji wangu Nitamjuvisha Kwa upungufu wangu Yeye anatosha; Majonzi yangu yote Na mizigo yangu, Atachukua vyote Yesu Bwana wangu.
Couplet 3
Na roho yangu nayo, Imechoka sana; Namletea hiyo Ilindwe na Bwana; Ni jema jina lake, Nalo lapendeza, Imanweli na kwake tutalitukuza.
Couplet 4
Natamani daima Niwe kama Bwana, Mpole, tena mwema, Wa mapenzi sana; Zaidi natamani Kwenda kwake juu, Nikaone Mbinguni Enzi yake kuu.