Indirimbo Zikundwa Open in the app

#47

Ni wako wewe

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Ni wako wewe, nimekujua, Na umeniambia; Lakini Bwana, nataka kwako nizidi kusongea.

Refrain

Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Pia damu ya thamani.

Couplet 2

Niweke sasa nikatumike Kwa nguvu za neema; Uyapendayo nami nipende, Nizidi kukwandama.

Refrain

Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Pia damu ya thamani.

Couplet 3

Nina furaha tele kila saa Nizungumzavyo kwako, Nikuombapo nami napata kujua nia yako.

Refrain

Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Sana, kwako mtini. Bwana vuta, vuta, nije nisongee, Pia damu ya thamani.

Couplet 4

Mapenzi yako hayapimiki, Ila ng’ambo ya liko. Anasa pia sitazijua, Bila kufika kwako.